Staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu.
Dar es Salaam: Mwisho wa malumbano!
Tofauti na inavyodaiwa kuwa staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’
alikiuka maagizo ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ya kutoka nje
ya nchi kufuatia kesi inayomkabili ya kifo cha mwigizaji Steven Kanumba,
Ijumaa Wikienda limechimba ukweli.
Hivi karibuni Lulu alikwenda nchini
Nigeria kuhudhuria Tuzo za African Magic Viewers Choice (AMVCA) aliibuka
mshindi wa Mtayarishaji wa Filamu Bora ya Afrika Mashariki (Mapenzi ya
Mungu).
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa
makarani wa mahakama hiyo aliyeomba hifadhi ya jina kwa kuwa siyo
msemaji wa mahakama hiyo alisema kuwa mawakili wa Lulu walimuombea
kibali cha kwenda Nigeria na kupewa kwani walitoa hoja za msingi ikiwemo
kwenda kuwakilisha taifa nchini humo.
Kwa upande wake Lulu alisema kuwa
hakutaka kuwajibu waliokuwa wakisema kuwa alikiuka maagizo ya mahakama
hiyo kwani haruhusiwi kusema lolote zaidi ya kuwaachia mawakili wake
ndiyo wenye jukumu hilo.
Ijumaa Wikienda lilizungumza na mmoja wa
mawakili wa Lulu, Peter Kibatala ambaye alisema kuwa walifuata
utaratibu zote ndipo mahakama ikatoa kibali kwa hoja kwamba alikuwa
anakwenda kuliwakilisha taifa.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )