Stori: Mwandishi Wetu, Zanzibar
UCHAGUZI wa marudio uliofanyika jana
Machi 20, Zanzibar umegawa wapiga kura kwani wapo waliodai kujitokeza
kupiga kura licha ya vyama vyao kupinga marudio ya uchanguzi huo na
wengine msimamo wao kubaki majumbani, Ijumaa Wikienda limegundua.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili
kisiwani Unguja umebaini kuwa, maeneo mbalimbali mjini hapo kumekuwa na
ulinzi wa polisi hali iliyoashiria kuwepo kwa tahadhari.
Maeneo kama Michenzani, Mji Mkongwe,
Mkunazini, Marikiti, Darajani, Magomeni, Uwanja wa Ndege, Shirika la
Utangazaji Zanzibar (ZBC) na Daraja Bovu, askari polisi walionekana
wakifanya doria kuimarisha ulinzi wakati wa zoezi la kupiga kura.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani
Omar Makame alipoulizwa kuhusiana na ulinzi huo alisema hilo ni jambo la
kawaida.“Hili ni jambo la kawaida, tunapaswa kulinda raia na mali zao…
ni jukumu la majeshi yote bila kujali mipaka ya kimajukumu,” alisema
Makame.Mwananchi mmoja aliyekataa kutaja jina lake lakini huku akidai
kuwa ni mfuasi wa Chama Cha Wananchi (CUF), alisema licha ya viongozi
wake kuwakataza kupiga kura, yeye aliamua kupiga kwa sababu ni haki yake
ya msingi.
“Mimi kupiga kura ni haki yangu ya
msingi na ya kikatiba. Sijakubaliana na walichosema viongozi wangu wa
CUF kwa sababu ni haki yangu ya msingi na kikatiba,” alisema mtu huyo
akiwa Mkunazini.
Uchaguzi wa Zanzibar ulipangwa kurudiwa Machi 20, mwaka huu baada ya ule uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha kwa madai kuwa, kulikuwa na kasoro nyingi.
Uchaguzi wa Zanzibar ulipangwa kurudiwa Machi 20, mwaka huu baada ya ule uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha kwa madai kuwa, kulikuwa na kasoro nyingi.
Nafasi zilizokuwa zikirudiwa kwa kura ni
kumchagua Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na
Madiwani. Oktoba 25, mwaka jana walipiga kura ya Rais wa Tanzania na
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )