Staa wa Ngoma ya Niroge, Vannessa Mdee
‘Vee Money’ kwa mara ya kwanza amefungukia kuchukizwa na baadhi ya watu
wanaomwita mwanamuziki wa kike.
Akichonga katika kipindi cha Exclusive
kinachorushwa na Global TV Online, Vee Money alisema kuwa angependa
kufananishwa na wanamuziki wengine wote na siyo kutengwa kwa kuwa
mwanamke basi atambulike kama mwanamuziki wa kike.
“Sawa naapenda muziki lakini
kinachoniuzi mara nyingi ni kutofautishwa na kuchukuliwa kama
mwanamuziki wa kike. Napenda kuujulikana kama mwanamuziki inatosha,”
alisema Vee Money.
Vannessa amezungumza mengi yanayomuhusu
yeye na maisha. alifanya mahojiano hayo kisha na kupiga picha na baadhi
ya wafanyakazi wa global publishers. Mahojiano kamili yanapatikana
keshokutwa Jumatatu kupitia www.globaltvtz.com
GPL
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )