Mkurugenzi
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna wa Polisi Diwani Athumani
amesema hadi kufikia sasa zaidi ya watu 150 wamejitokeza kuhakiki wa
silaha zao, katika hatua ya kutii agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda.
“Baada
ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kufanya uhakiki wa silaha
zake hivi karibuni, watu zaidi ya 150 wakiwemo viongozi mbalimbali
waliopo Serikalini, Viongozi wastaafu, Mabalozi wa nchi mbalimbali,
wafanyabiashara na wabunge wamejitokeza kuhakiki silaha zao, na
wengine wameonesha nia ya kufanya hivyo, hata hivyo tusingependa kutaja
majina yao kwa sababu za kiusalama” amesema Kamishna wa Polisi Athumani
Athumani
amesema kuwa, lengo la kufanya uhakiki wa silaha ni pamoja na kuboresha
hali ya usalama na kuwajua watumiaji, kuwatambua tena wamiliki wa
silaha pamoja na kuwa wanawatambua isipokuwa zinaweza kutokea sababu
mbalimbali zitakazofanya wasiendelee kumiliki silaha hizo ikiwemo vifo
na ulemavu na kusema kuwa wangependa kufahamu taarifa za namna hiyo,
ameongeza kuwa zoezi hili sasa ni la nchi nzima si kwa Mkoa wa Dar es
Salaam pekee kama ilivyokuwa hapo awali.
Aidha,
wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam wanaweza kuhakiki silaha zao katika
vituo vya Osterbay Polisi, Temeke Chang’ombe Polisi na Ilala central
Polisi, ambapo wanatakiwa kwenda na kitabu(firearm licence book),
picha ndogo nne za mhusika, pamoja na anwani sahihi ya mahali
anapoishi mhusika.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )