Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Geofrey Mungereza akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwanamuziki wa BMM Band, Totoo Zebingwa, akielezea kero anazokumbana nazo kwenye tasnia hiyo.
Prezidaa wa Bendi ya Soundton Sound, Mackey Fanta, akinyoosha mkono wakati akitaka kutoa lake la moyoni.
Waziri Nape akimpongeza Mzee Makassy kwa kazi nzuri aliyoifanya kwenye tasnia hiyo tangu enzi hizo.
Mwanamuziki wa Woman Band iliyowahi kutamba miaka ya nyuma, Bi Kitenge, akimwomba waziri awakumbuke na wao.
Mkongwe, Shaaban Dede, akitoa kilio chake na uduni wa muziki huo.
Prezidaa wa FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Nyoshi El Saadat, akitoa mapendekezo ya kuboresha muziki huo.
Mdau wa muziki wa dansi nchini, Said Mdoe, naye akitoa yake ya moyoni.
Waziri Nape akijibu hoja mbalimbali zilizochangiwa kwenye mkutano huo.
WAZIRI wa Habari, Vijana, Sanaa Utamaduni na Michezo, Nape
Nnauye, leo alizungumza na wanamuziki wa dansi na kusikiliza vilio vyao
ambapo aliwaahidi kuyatatua baadhi ya matatizo yaliyo ndani ya uwezo
wake.
Katika mkutano huo uliofanyika Ukumbi wa CCM Vijana uliopo Kinondoni,
mamia ya wanamuziki hao walihudhuria wakiwemo wakongwe waliotamba enzi
hizo akiwemo Mzee Makassy, King Kikii, Mzee Manyema, Komandoo Hamza
Kalala na wengineo.
Wanamuziki hao walielezea mambo kadhaa yanayoudumaza muziki huo na
kuwaacha masikini licha ya kuwa na majina makubwa. Miongoni mwa kero
hizo ni pamoja na ‘kubaniwa’ nafasi kwenye vyombo vya habari, kukosa
msimamizi mwaminifu wa kuuza kazi zao baada ya kuzirekodi na mengineyo.
PICHA : RICHARD BUKOS / GPL
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )