Wema Sepetu ni bingwa wa kutumia gharama kubwa kufanya filamu na kutengeneza kiu kubwa kwa mashabiki wake halafu then mradi unageuka kuwa kama album ya Detox ya Dr Dre, ambayo haijawahi kutoka hadi leo.
June 2012: Muigizaji wa Nigeria, Omotola Jalade akiwa na Wema baada ya kuwasili kutoka Nigeria kuhudhuria uzinduzi wa filamu ya Superstar ambayo hadi leo haijatoka
Miaka minne iliyopita, Wema alidai
kutumia mamilioni ya shilingi kufanya filamu aliyoipa jina ‘Superstar.’
Na hata uzinduzi wake uliofanyika Hyatt Regency Hotel (Kilimanjaro)
ulikuwa wa kifahari na wa aina yake. Mastaa karibu wote wa Tanzania
walialikwa na kuona sehemu ya filamu hiyo.
Alitisha zaidi kwa kumleta msanii nguli
wa Nigeria, Omotola Jalade aliyeshuhudia uzinduzi huo. Bahati mbaya hadi
leo filamu hiyo haijawahi kutoka sokoni na mrembo huyo aliamua
kuifungia kabatini.
Tupeleke mbele. Mwaka jana Wema alienda
Ghana na kufanya filamu na staa wa huko, Van Vicker iitwayo ‘Day After
Death’. Filamu hiyo ilifanyika December 2014. Kwa mujibu wa ratiba ya
mwisho, ilikuwa itoke September mwaka jana.
Meneja wake, Martin Kadinda, alidai ilishindikana kutoka kwasababu ya kampeni za uchaguzi.
“Filamu mpaka sasa ipo tayari, lakini
movie hii hatuwezi kuiachia kama anavyoachia movie nyingine.Lazima
afanye launch na ilikuwa launch ifanyike toka mwezi wa tisa lakini toka
mwezi wa sita mpaka sasa Wema yupo kwenye kampeni,” Kadinda aliiambia
Bongo5.
“Kwahiyo tunasubiri mpaka hizo kampeni
ziishe na uchaguzi upite Wema atakuwa anazindua products zake mpya
halafu baada ya hizo products kuzinduliwa ndio filamu itazinduliwa
rasmi,” aliongeza.
Lakini hadi sasa hakuna dalili za filamu
hiyo kutokana na haiongelewi tena? Kunani? Tuna wasiwasi kuwa filamu
hii inaweza kuungana kabatini na Superstar zikipeana moyo.
Bongo 5
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )