Msanii
mkongwe wa muziki kutoka Morogoro Afande Sele, amesema 20 Percent
anateswa na tuzo tano za Kili Music Awards alizochukua mwaka 2011 ndio
maana kila akitoa wimbo unashindwa kufanya vizuri.
Akizungumza
katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television Alhamisi hii,
Afande amesema 20 Percent toka achukue tuzo, ameshindwa kabisa kurudi
kwenye muziki.
“Ni
kweli zinamtesa mimi naamini hivyo. Kwa hiyo nathubutu kusema zimemtesa
na zinaendelea kumtesa,” alisema Afande. 20 Percent ameshajaribu kutoa
nyimbo kadhaa lakini zimeshindwa kuteka hisia za mashabiki wake kama
nyimbo zake za zamani.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )