Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo amesema kuwa kwa Tanzania
kutopatiwa fedha na Marekani kupitia Mfuko wa Maendeleo ya
Changamoto za Milenia (MCC) ambazo ni Dola za Marekani milioni 472 kwa
ajili ya miradi ya barabara, maji na umeme hazitaathiri miradi ya
usambazaji umeme vijijini inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati
Vijijini (REA).
Aliyasema
hayo jijini Dar es salaam wakati akifanya majumuisho ya vikao vyake
na wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini ambavyo vilianza tarehe 29
Machi, 2016 na kuhudhuriwa na watendaji wa Wizara, Shirika la Umeme
Nchini (TANESCO) na REA.
Profesa
Muhongo alisema kuwa fedha hizo zilikuwa haziendi moja kwa moja katika
mfuko wa REA wala serikali kuu kama inavyodaiwa na watu wengi.
“Zile
fedha za MCC tulikuwa tunakaa na MCC, tunasema bwana katusaidie
kusambaza umeme mfano Shinyanga, kwa hiyo anachukua zile fedha zake
anaenda na wakandarasi wake moja kwa moja Shinyanga, huku miradi ya REA
ikiendela kama ilivyopangwa, ”alisema Profesa Muhongo.
Alisema
kuwa miradi ya MCC ilikuwa ikisaidia juhudi za serikali katika
kusambaza umeme vijijini na mijini lakini fedha hizo zilikuwa
hazipelekwi REA.
Alisisitiza
kuwa kabla ya MCC kuanza kutoa fedha za kuendeleza miradi ya umeme,
serikali tayari ilikwishaanza kusambaza nishati hiyo kwa wananchi na
kwamba kuna wadau mbalimbali wanaochangia miradi hiyo na hata kama
wasipochangia, jukumu la serikali la kuwasambazia wananchi wake umeme
linabaki kuwa pale pale.
“Isichukuliwe
kwamba fulani asipochangia, sasa taifa zima miradi yake imekufa, hivyo
dhana ya kusema kwamba fedha hizo zilikuwa zinapelekwa REA ni
upotoshwaji wa hali ya juu, kwamba REA itaathirika kwa kukosa hizo
fedha si kweli,” alisema Profesa Muhongo.
Akielezea
utekelezaji wa miradi ya REA awamu ya pili, Profesa Muhongo alisema
awali jumla ya shilingi bilioni 881 zilitengwa lakini zikaongezeka
shilingi bilioni 60 ambapo hadi kukamilika kwa awamu hiyo ya pili
jumla ya vijiji 2500 vinatarajiwa kupata umeme, huku wateja wa awali
250, 000 kuunganishwa na huduma hiyo hadi kufikia mwezi Juni, mwaka
huu ambao ni ukomo wa utekelezaji wa awamu hiyo.
Kuhusu
tathmini ya wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini, Profesa Muhongo
alisema kuwa wakandarasi wengi wametekeleza miradi hiyo kwa asilimia
kati ya 75 na 85, huku wengine wakivuka wastani wa REA ambao ni
asilimia 87.
Katika
hatua nyingine, Profesa Muhongo alitoa miezi miwili kwa wakandarasi
ambao hawajakamilisha miradi na kusisitiza miradi yote kukamilishwa
mwezi Mei au Juni 15, mwaka huu kabla ya kuanza kwa awamu ya tatu
inayotarajiwa kuanza ifikapo Julai mosi mwaka huu.
Aliongeza
kuwa katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, serikali
imebaini kuwa wapo wakandarasi wanaotumia vifaa hafifu kama transfoma
na nguzo na kusisitiza ukaguzi kufanyika na kampuni itakayobainika
kutumia vifaa hafifu itafutwa mara moja kabla ya awamu ya tatu.
Ili
kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi, Profesa Muhongo aliitaka TANESCO
kwa kushirikiana na Wizara kuhamasisha wananchi hasa waishio vijijini
kujiunga na huduma ya umeme, na TANESCO kusogeza huduma karibu na
wananchi ili kuepusha wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya
kuunganishiwa umeme au changamoto nyingine zinazotokana na nishati
hiyo.
Akizungumzia
kuhusu malipo ya wakandarasi hao, Profesa Muhongo alisema kuwa serikali
imeendelea kulipa wakandarasi wote kwa wakati kulingana kazi
zinazofanyika.
Wakati
huo huo Profesa Muhongo alisema kuwa mitambo ya kuzalisha umeme kwa
kutumia gesi asilia ya Kinyerezi I kwa sasa inazalisha Megawati 150 na
kuongeza kuwa malipo kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya Kinyerezi II
inayojengwa na kampuni ya Sumitomo kutoka nchini Japan yameshakamilika
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )