Featured
Loading...

Anayemmaliza Ray C, Huyu Hapa


vlcsnap-908345Kijana Frank akiwa chakali.
Hali mbaya! Mwanaume anayeonekana pichani anaitwa Frank. Katika habari hii tunamtaja kwa jina moja tu, Risasi Mchanganyiko linakwambia yeye ni nani!
SASA FRANK NI NANI?
Frank anatajwa kuwa, ndiye aliyechangia kwa sehemu kubwa kumrudisha msanii wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ katika utumiaji wa madawa ya kulevya ’unga’.
Katika Gazeti la Ijumaa Wikienda ambalo ni ndugu wa damu na hili la juzi Jumatatu, ukurasa wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa kisemacho; RAY C ANASWA KAZIMIKA!
MSINGI WA HABARI
Habari hiyo ililenga kuonesha ni namna gani msanii huyo amerejea katika matumizi ya unga baada ya kumwathiri miaka mitatu iliyopita na kupata matibabu kwenye kitengo cha waathirika wa unga Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu wa Kinondoni, Mwananyamala jijini Dar.
vlcsnap-908424ALITOKEA ARUSHA
Simulizi inasema kuwa, Frank ni mwenyeji wa jijini Arusha ambako wazazi wake wanaishi huko lakini kiasili ni mtu wa kutoka Mkoa wa Mbeya.
ALIKUJAJE DAR?
Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka Hospitali ya Mwananyamala, Frank aliwasili jijini Dar mwanzoni mwa mwaka huu kwa lengo la kupata tiba ya dawa za Methadone ambazo hutumiwa na waathirika wa unga.
“Akiwa anatumia dozi hiyo, inaonekana pia alikuwa akiendelea na unga. Ndiyo tatizo la waathirika wengi wa madawa ya kulevya. Haitakiwi kuchanganya jamani.
Wanapochanganya, wanashindwa kupona.
“Sasa sijui ilikuaje, ghafla akakutana na Ray C na kuanza kushikamana kama marafiki wakubwa. Ray C naye, kipindi hicho alikuwa anatumia Methadone, lakini naye hakuacha unga. Nasikia pia wakawa wapenzi,” kilisema chanzo hicho kikiomba hifadhi ya jina lake kwa vile si msemaji wa hospitali hiyo.
IMG-20160325-WA0000Frank na Ray C wakiwa hoi chakali.
TUKIO LA KARIBUNI
Chanzo kinaendelea: “Sasa juzikati tu hapa, Frank yakamkuta mazito. Akiwa maeneo ya Mwananyamala, tena peke yake, alizidiwa na unga na kujikuta akizimika.
“Baadhi ya watu walipomwona, waliamini jamaa ameugua ghafla na yuko na hali mahututi, wakambeba na kumkimbiza Hospitali ya Mwananyamala ili kuokoa maisha yake.
“Bahati mbaya ni kwamba, alifikishwa pale madaktari wakiwa wameshaondoka. Lakini kutokana na hali yake kuwa mbaya, muuguzi mmoja alimpigia simu daktari na kumjulisha. Akaambiwa kama atachelewa, anaweza asimkute jamaa. Ikabidi arudi na kumpatia matibabu.”
WANAOMJUA FRANK
Baadhi ya watu wanaomjua kijana huyo wameliambia gazeti hili kuwa, mwonekano, Frank anafanana sana na Mbongo Fleva, Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ ambaye ndiye mwanaume wa kwanza kutajwa kumfundisha Ray C kubwia unga.
IMG-20160325-WA0001
MAMA RAY C ATAFUTWA
Juzi, gazeti hili lilimpigia simu mama yake Ray C, Margaret Mtweve ili kujua Ray C anaendeleaje na afya yake baada ya hivi karibuni kunaswa akiwa amezima, lakini simu ya mama huyo iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
KINACHOWAMALIZA CHAJULIKANA
Kwa mujibu mwa muuza unga mmoja ambaye jina lake linafichwa, aliliambia gazeti hili kuwa wavutaji wengi wa Bongo wanatumia cocaine kutoka Pakistan na Afghanistan, inayojulikana zaidi kama Musharaf, ambayo ni hafifu na yenye kuuzwa bei rahisi.
“G moja (G ni ujazo wa gramu moja) ya Musharaf inauzwa kwa shilingi kati ya 23,000 hadi 25,000 ambayo inaweza kutoa ‘pinch’ (kipimo cha chini kabisa kinachouzwa kwa watumiaji wa aina ya akina Ray C) kati ya 20-40. Cocaine kutoka Brazil, ambayo ndiyo bora, inayoitwa na watu wa unga kama Mchezaji au Pele, inauzwa kwa shilingi kati ya 50,000 hadi 60,000 kwa G moja.”
BOFYA HAPA UPATE ZAIDI
“Matajiri wengi wa Kihindi, Waarabu na Waswahili kama f’lani (anatajwa mfanyabiashara mkubwa) wanatumia cocaine ya Pele ambayo haitaki kabisa uchafu, ndiyo maana unawaona wako fresh kabisa.
“Ile Musharaf inakuwa mbaya zaidi kwa sababu wauzaji wa hapa wanachanganya na Baking Powder (Hamira) ili iwe nyingi na hivyo kutoa pinch nyingi zaidi.”
00301047-b58ba41202d313a9834230ea50e40135-arc614x376-w1200
HUYU HAPA MKEMIA
“Baking poda iliyochanganywa kwenye madawa ya kulevya kama cocaine ina madhara makubwa kwenye mwili wa binadamu iwapo itatumiwa kwa muda mrefu au kwa kiwango kikubwa. Baada ya kuingia kwenye mwili wa binadamu, baking poda huvunjwavunjwa na kutengenezwa madini chumvi ya sodiamu na carbonate ambayo huchukuliwa moja kwa moja kwenye mzunguko wa damu.
“Hii husababisha kuongezeka kwa kiwango cha madini chumvi ya sodiamu (ambayo yamo ndani ya baking poda) tofauti na kiwango kinachotakiwa kwenye mwili.
“Madhara makubwa ya matumizi ya baking poda kwenye mwili wa binadamu ni mishipa ya damu kushindwa kufanya kazi, ugonjwa wa moyo, kuongezeka kwa kiwango cha sukari mwilini (hyperosmolar), maji kuzidi kwenye damu kuliko kiwango cha kawaida (hypervolemic), kuongezeka kwa sodiamu na kupungua kwa maji mwilini kuliko kawaida (hypernatremia),” alisema mkemia huyo aliyejitambulisha kwa jina la Lindege.
GPL

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top