Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwanaisha Nyange ‘Dayna Nyange’.
MWANADADA anayefanya poa kwenye gemu la
Muziki wa Bongo Fleva, Mwanaisha Nyange ‘Dayna Nyange’ hivi karibuni
amedai kuwa anamuona wivu staa wa Hip Hop, Roma Mkatoriki kutokana na
hatua aliyoifikia ya kufunga ndoa Jumamosi iliyopita mkoani Tanga na
mchumba wake wa muda mrefu.
Dayna anasema amekuwa mtu wa karibu wa
Roma kwa muda mrefu sasa ambapo amewafahamu wapendanao hao tangu mwaka
2008 na anashukuru kuona wametimiza ahadi yao ya kuoana lakini kwake pia
hiyo ni changamoto ya kuhakikisha pia anaingia kwenye ndoa.
“Roma amefanya kitu cha msingi,
ninamuonea wivu kuingia kwenye maisha ya ndoa na ninafikiri
amenikumbusha pia kutakiwa kulitimiza hilo jukumu,” alisema Dayna.
Nyange.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )