Diamond
amesema hataki kuulizwa tena kama ana bifu na msanii mwingine, amedai
hana tatizo na msanii yoyote na ndio maana hata ukienda ofisini kwake
utakuta ameweka picha za wasanii wote hata ambao amekuwa akihusishwa
kuwa na bifu nao.
“Ukija
ofisini kwangu me nna kuna picha ya blue nimembandika, kuna picha ya
Juma Nature, kuna picha ya Ali , kuna picha ya Prof, Jay, kuna picha ya
Ray C, kuna picha ya Q chief, TID, AY, wasanii wote wakubwa ambao anajua
walianza katika huu muziki, wana mchango katika huu muziki wote me
nimewaweka” Diamond aliiambia AyoTv.
“Ofisini
kwangu tu ukiingia tu reception, ukiingia tu kunasehemu nimeweka picha
za wasanii wote , siwezi kuweka wote kwasababu zisingetosha lakini kuna
baadhi ya wasanii nimeweka kwasababu najua wanamchango kwenye soko la
muziki wa Tanzania.” Diamond alielezea
Diamond pia amesema kuwa yeye ndio huwa anahushishwa na bifu na wasanii wengine lakini yeye hana tatizo na mtu
Source: AyoTv
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )