Featured
Loading...

Ray c anaswa…

IMG-20160325-WA0002
Stori:  Musa Mateja, Wikienda
DAR ES SALAAM: LICHA ya kutumia nguvu nyingi kukanusha habari zinazochapishwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers kuwa, amerejea kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’, hatimaye staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amenaswa ‘laivu’ akiwa ‘ameangusha gari’ kando ya barabara, habari ndiyo hiyo!
Ray C ambaye kila anapoandikwa na Magazeti ya Global kuhusu kurejea kwenye unga, amekuwa akimtupia shutuma Mkurugenzi wa Global, Eric Shigongo kwamba anamchafua, alinaswa na mapaparazi wetu hivi karibuni maeneo ya Mwananyamala Magengeni, Dar akiwa amezima yeye na mwanaume aliyekuwa naye hali iliyompa urahisi paparazi wetu kuwafotoa picha za kutosha.
ISHU ILIANZA JANUARI
Januari mwaka huu, gazeti hili liliripoti habari iliyokuwa na kichwa; CHIMBO LA UNGA LA RAY C LAGUNDULIKA.
Baada ya habari hiyo kutoka, Ray C aliikanusha kupitia ukurasa wake wa Instagram akisema:
“Seriously kwa kweli huwa naumia sanasana kuona binadamu mwenzangu anadiriki kuniharibia jina langu ili yeye apate kula! Hamjui mnaniathiri kiasi gani na hizi habari zenu! Hiyo habari yaani ni ujingaujinga tu umeunganishwa na picha yangu bila hata uoga mmeichukua kutoka kwenye page yangu ya Insta. Mnazitumia kunichafulia jina langu tena wakati ndiyo kwanza nahangaika kurudi kwenye kazi yangu.”
IMG-20160325-WA0000TV ANDAGRAUNDI IKAMSAPOTI
Kama hiyo haitoshi, kituo kimoja cha runinga cha muda mrefu nchini lakini bado kiko ‘andagraundi’ kilimpa nafasi Ray C akanushe habari ya Ijumaa Wikienda pasipo kujua gazeti hili lilijiridhisha kabla ya kuandika habari hiyo.
SHIGONGO ATAKA UKWELI
Baada ya Ray C kuyaponda Magazeti ya Global kwenye runinga kwa kudai yanamchafua, Shigongo alimuagiza Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Oscar Ndauka kupanga makachero kutokea kwenye kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ili kufuatilia nyendo za msanii huyo kama kweli anaonewa au la na kutaka matokeo yaliyo kamili!
OFM KAZINI
Timu ya OFM ilipangwa kwa zamu kumfuatilia Ray C kwa saa ishirini na nne ili kujiridhisha juu ya malalamiko yake, hasa kwamba Global inaungaunga picha za zamani ili kupata habari kama alivyosema kwenye Instagram yake.
Tangu Januari hiyo, timu ya OFM ilianza kuwa sambamba na Ray C huku makachero wengine wakiwasaka watu wake wa karibu ili kusikia chochote kutoka kwao.
MSIKIE HUYU
“Mimi ni miongoni mwa watumiaji wa madawa ya kulevya ambaye nilishawishiwa na Ray C kuacha na kunileta hapa kwenye Kituo cha Mwanayamala (hospitali) kwa ajili ya kuanza kumeza Methadone (dawa za kuponya waathirika wa madawa ya kulevya) ili niweze kurudia hali yangu ya kawaida. Hali yangu sasa niko safi na najitambua.
IMG-20160325-WA0001AMSIKITIKIA RAY C
“Kinachoniuma ni Ray C ambaye aliniunganisha hospitali kwa mbwembwe, yeye ameshindwa kuendelea na kapata bwana ambaye amemsaidia kurudia tena matumizi ya unga kushinda zamani. Huwezi amini kwa sasa mwenzetu gari limewaka upya, anawasumbua hata madaktari wetu, wakati mwingine wamekuwa wakishindwa kumhudumia.
FULL VURUGU
“Akija hapa kituoni kuchukua dawa muda wote ni kuwasimanga hawa wauguzi wetu jambo ambalo linatukera sana kwani anatuharibia hata sisi ambao alituleta. Aliyemponza ni Frank. Frank alikuja hapa kituoni kama mwathirika na kuanza kutumia dawa.
“Baada ya kukutana na Ray C na kuwa marafiki, wameshindwa kuendelea kutumia dawa. Badala yake wamekuwa wakivuta unga kiasi cha kuzima na kuleta fujo tu. Huyu Frank anaishi Mwananyamala karibu na hapa hospitali,” alisema mwathirika mmoja akiomba kufichiwa jina lake.
MADAKTARI WALIMSUSA
Akaendelea: “Unajua  madaktari wa hapa  walifikia hatua ya kujivua kumhudumia na kumrejesha kwao kipindi kile alipofanya fujo Posta. Ninasema haya kwa uchungu maana hata sisi tunaokunywa naye dawa hakuna hata mmoja anayeweza kummudu zaidi ya huyo Frank ambaye naye gari limeshachanganya, anampoteza kabisa Ray C,” kilisema chanzo hicho.”
JK ANYOOSHA MIKONO, AMUACHIA MAGUFULI
Chanzo kingine kilichopo kwenye hospitali hiyo kililiambia Ijumaa Wikienda kuwa, kutokana na JK kumsaidia alipokuwa madarakani na mrembo huyo kurejea tena kwenye unga, amenyoosha mikono, jukumu hilo litabaki kwa rais wa sasa, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’.
IMG-20160325-WA0004“JK ameshanyoosha mikono. Hawezi tena kumuelewa huyu dada, amemuachia Magufuli naye labda ajaribu kwani ndiye aliyeko madarakani,” kilisema chanzo hicho.
RAY C MWENYEWE HUYU HAPA
Alipotafutwa Ray C juzi na kusomewa madai hayo na kuelezwa juu ya kupigwa picha zinazomuonesha akiwa amezima, alifunguka:
“Kweli kuna picha nimesikia watu walinipiga nikiwa nimezimika lakini siyo kwamba nilivuta unga kiasi hicho, picha hizo nilipigwa kweli nikiwa nimezima baada ya kunywa dawa hapo hospitali maana dawa ninazokunywa huwa ni kali sana, saa nyingine huwa nashindwa kujizuia na kujikuta nimezima.
“Kwanza unatakiwa ujue kwamba hizi dawa siku zote ukinywa hata kama ungekuwa na nguvu kiasi gani lazima kuna muda unafikia hatua ya kushindwa kabisa kujimudu na saa nyingine huwa tunalala hata na wenzangu kwani hata hizo picha wamenipiga chini ya mti hapahapa jirani na eneo la hospitali, siku hiyo nilikuwa nimezidiwa sana.”
AMTAJA FRANK KAMA ‘BEBI’ WAKE
“Ninachokijua nilala chini ya mti na Frank lakini hata ukiangalia nyuma yetu pia
kuna watu kibao ambao nao walikuwa wamelala baada ya kunywa dawa na kuzidiwa, sasa sijui wewe hizo zangu na huyo mpenzi wangu umezitoa wapi,” alisema Ray C.
DAKTARI WA WAATHIRIKA AZUNGUMZA
Baada ya utetezi huo wa Ray C, gazeti hili lilimwendea hewani daktari wa tiba kwa waathirika na unga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (jina lipo) na kumuuliza kama matumizi ya dawa za Methadone yanaweza kumzimisha mtumiaji ambapo alisema:
“Kama anayetumia Methadone baada ya kuathirika hatatumia madawa ya kulevya hawezi kuzima kwa namna yoyote ile. Ukimwona mtu anazima ujue anachanganya, yaani anameza Methadone pia anaendelea kubwia unga.”
TUMEFIKAJE HAPA?
Ray C aliyewahi kutamba na nyimbo nyingi kali, ikiwemo Na Wewe Milele, alijikuta ametopea kwenye madawa ya kulevya baada ya kutumbukia kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa staa wa Hip Hop Bongo, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ ambaye naye anadaiwa kutumia.
Baadaye wawili hao walimwagana huku Ray C akichanja mbuga katika eneo hilo hali iliyomlazimisha ‘kustaafu’ muziki kutokana na mwili kukosa mawasiliano katika kupanga mikakati.
Gazeti damu moja na hili, Ijumaa, toleo Namba 799 la Novemba 2-8, 2012 lilitoa picha za Ray C akiwa amezimika na habari yenye kichwa; DAH!
RAY C. Tukio hilo lilijiri maeneo ya Magomeni, Dar.
JK ASOMA, APATA UCHUNGU
Wiki moja baada ya gazeti hilo kuingia mtaani likielezea hali ya Ray C, JK alimwita Ikulu ya Dar es Salaam yeye, mama yake mzazi, Margaret Mtweve na ndugu mwingine hali iliyoonesha kuwa, aliisoma habari hiyo kwenye Gazeti la Ijumaa.
Lengo la kumwita lilikuwa kumsaidia mwanamuziki huyo kwa tiba na uangalizi wa kina jambo ambalo lilifanyika na akarudia kwenye hali yake ya kawaida.
Mwaka 2015, baada ya minong’ono mingi kwamba msanii huyo amerejea katika matumizi ya unga, magazeti ya Global yaliandika habari hiyo na Ray C akawa anakanusha mara kwa mara mpaka majuzi aliponaswa akiwa amezima.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top