Featured
Loading...

Maafa ya Mafuriko..Mwanafunzi Asombwa na Maji Akiogelea Morogoro

 
Morogoro. Mwanafunzi wa chekechea wa Shule ya Msingi ya Dala iliyoko Kata ya Mvuha, Erick Makale (6) amefariki dunia baada ya kusombwa na mafuriko wakati akiogelea na wenzake kwenye Mto Mvuha mkoani hapa.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu, mwenyekiti wa kijiji hicho, Boi Lubegete alisema kuwa mwili wa Erick bado haujaonekana.

Lubegete alisema kuwa Erick alikuwa na wenzake watatu na waliingia kuogelea mtoni baada ya kumaliza kazi ya kufua, lakini yeye aliingia kwenye kina kirefu na ndipo aliposombwa na maji.

“Watoto wenzake walieleza kuwa baada ya Erick alijaribu kujiokoa kwa kushika mti kando ya mto huo, lakini baadaye aliuachia na kuzama. Mpaka leo bado mwili wake haujapatikana,” alisema Lubegete.

Wakati huo huo Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini imetoa msaada wa vyakula vyenye thamani ya Sh3.5 milioni kwa kaya 86 zilizoathiriwa na mafuriko.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top