Mamia ya watu wamekongamana nje ya uwanja wa ndege wa Kinshasa kuupokea mwili wa mwanamuziki Papa Wemba uliowasili nchini humo kutoka Abidjan
Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya mwili huo kuwekwa katika uwanja wa mpira kwa raia kutoa heshima zao za mwisho.
Maafisa wa serikali na wanadiplomasia watahudhuria ibada ya kumkumbuka mwanamuziki huyo katika uwanja wa ndege kabla ya mwili huo kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Tamasha la bure la usiku kucha lilifanyika mjini Abidjan ambapo mwanamuziki huyo alianguka alipokuwa akiimba.Mwanahabari wa BBC Tamasin Ford anasema kuwa mashabiki wengi walivalia nguo nyeusi na kubeba mishumaa ili kutoa heshima kwa nguli huyo wa muziki.
Mkewe Papa Wemba na wasaidizi wake pia walikuwepo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )