Alisema, CCM itafanya hivyo kwa sababu kazi anayoifanya ya kupambana na wazembe na wezi wa mapato kwenye vyanzo vya uchumi wa taifa inatokana na maelekezo ya ilani ya CCM.
Sendeka alisema, CCM inawataka wale wote wanaojaribu kupotosha jitihada zinazofanywa na Rais za ‘kupasua majipu’ wakidai kuwa ni kuwaonea wanaochukuliwa hatia, kuacha mara moja, kwa sababu kinachofanyika ni sahihi na kipo kwa mujibu wa sheria.
Alisema, upasuaji majipu huo unaofanaywa na Rais Magufuli hauchagui chama bali yeyote anayebainika kuwa ni jipu hata akiwa mwana CCM haachwi.
Kwa upande wake, Mjumbe wa NEC, Kilumbe Ng’enda, aliwataka Watazania kutambua kuwa Uchaguzi umeshamalizika kwa hivyo asitokee yeyote kuanza kuweweseka, kwa kutoa maneno ya kejeli kuhusu utendaji kazi wa Rais Dk. Magufuli kwa sababu baada ya uchaguzi kumalizika sasa kiichobaki ni kuchapa kazi.
Alisema, hakuna sababu za mwanasiasa yeyote kuanza mambo ya fitina za kisiasa wakati huu kwa kuwa kufanya hivyo ni kujisumbua
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )