Dar es Salaam: Msiba! Tasnia ya Muziki
wa Dansi Bongo imegubikwa na simanzi nzito kufuatia kifo cha aliyewahi
kutikisa vilivyo kwa rap na vibao vikali, mwenye asili ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Ndanda Kosovo ‘Kichaa’ aliyefikwa na umauti
wikiendi iliyopita, Wikienda limechimba undani wa habari hiyo.
Habari zilizolifikia Wikienda mara tu
baada ya kutokea kwa msiba huo asubuhi ya Jumamosi iliyopita zilieleza
kuwa, Ndanda alisumbuliwa na tumbo ambapo alilazwa kwenye Hospitali ya
Mwananyama na baadaye kuhamishiwa Muhimbili jijini Dar.
Akizungumza na Wikienda, mjomba wa Ndanda ambaye pia ni mwanamuziki, Cardinal Gento alisema kuwa, Ndanda alihamishiwa Muhimbili baada ya tatizo lake kushindikana Mwananyamala.
Akizungumza na Wikienda, mjomba wa Ndanda ambaye pia ni mwanamuziki, Cardinal Gento alisema kuwa, Ndanda alihamishiwa Muhimbili baada ya tatizo lake kushindikana Mwananyamala.
“Nilikesha naye hospitalini, ilipofika
asubuhi nikaondoka kurudi nyumbani kwa ajili ya chakula, nikaacha
anafanyiwa mpango wa damu maana alikuwa amepungukiwa, lakini muda mfupi
baada ya kuondoka, nikapigiwa simu amefariki dunia,” alisema Gento
wakiendelea na utaratibu wa msiba nyumbani kwa Ndanda, Madale, Dar.
Kabla ya kukutwa na umauti, historia ya
ugonjwa wake inaonesha ilianza mwaka jana ambapo aliripotiwa na Magazeti
ya Global kuwa alilazwa kwenye Hospitali ya PKA iliyoko Tegeta, Dar
akisumbuliwa na tatizo la kupasuka kwa mmoja wa mishipa tumboni hivyo
kutapika damu.
HISTORIA FUPI YA NDANDA KOSOVO
Ndanda aliwika na Bendi ya FM Academia International ambapo alitunga nyimbo za FM Academia baada ya kutoka jela akiwa na akina Nyoshi El-Sadaat, Maluu Stonch, Mulemule FBI, King Blaize, Patcho Mwamba, Gento na wengine kibao waliotamba na Wimbo wa Wajelajela.

Baadaye Ndanda alitoka FM Academia
International akaanzisha Bendi ya Stono Musica akiita Wajelajela
Original akiwa na Maluu, Chai Jaba, Patcho na wengine. Miongoni mwa
nyimbo zake zilizotamba ni pamoja na Binadamu pamoja na rap zake za
Kidedea na Kaokota Big G.
Baadaye Ndanda aliachana na Stono Musica
akaelekea Marekani kwa shughuli za kimuziki ambazo zilikuwa na mafaniko
makubwa. Aliporejea Bongo ndipo akaanzisha Kundi la Watoto wa Tembo
kabla ya kuachana na bendi na vikundi na kuwa msanii anayejitegemea.
-GPL
-GPL
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )