Ni msanii
ambaye aliibuka kupitia filamu ya This is it akiwa sambamba na mwigizaji
mwenzake Jenifer huyu si mwingine ni Othuman Njaidi ‘Patrick’ vipaji
vilivyoiburiwa na maremu Kanumba Patrick anasema kuwa anamkumbuka sana
Kanumba kwani alikuwa mlezi kwake.
“Ni tofauti
sana na Uncle Kanumba alivyotulea, yeye alitulea kama watoto wake kazini
lakini watayarishaji wengine hawatupi nafasi hiyo wananichukulia kama
mwigizaji tu na wala sina ndoto nyingine,” Patrick
“Kila mara
ninapomkumbuka Uncle Kanumba ni tofauti kabisa na watayarishaji wengine
ambao wanatuchukulia kama wasanii wengine na si watoto tunaohitaji
kulelewa vema, kwa kutumia siku ya kumbukumbu ya kifo chake
tunafarijika,”
Patrick anasema
kuwa marehemu aliwachukulia kama familia yake huku akiwahimiza kusoma
kwa bidii na kutenganisha muda wao kufanya kazi za sanaa na muda wa
shule lakini wengi wanakuwa ubanaji wa muda msanii huyu yupo kidatu cha
nne Kifai Mordern School Kilvya.
Kesho ni siku
ya tarehe 7. April. ambayo mwigizaji mahiri katika tasnia ya filamu
Swahilihood Steven Kanumba ‘Kanumba the Great’ alifariki dunia, kifo
kinachosadikiwa kusababishwa na msanii mwezake wa kike Elizabeth Michael
‘Lulu’ ni siku muhimu kwa wasanii wote Bongo kumkumbuka gwiji huyo .
Kesho majira ya
saa tisa katika makaburi ya Kinondoni familia ya Kanumba na wasanii
wenzake watafanya kumbukumbu kwa ajili msanii huyo kipenzi cha wapenzi
wa filamu.
FC
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )