NIKIRI wazi, simjui ki-hivyo Vanessa
Mdee, ‘Vee Money’, ila kama mdau wa muziki, naheshimu kazi zake chache
alizofanya, ambazo zimemuweka katika daraja lenye hadhi katika Bongo
Fleva.
Licha ya umri wake mdogo (amezaliwa Juni 7, 1988) anaonekana amefanya mambo mengi makubwa, yakiwemo kufanya kazi katika vyombo kadhaa vya habari alipohusika kuwahoji watu wengi maarufu duniani, kutoa neno katika mikutano mikubwa ya kimataifa ya vijana iliyofanyika katika mataifa mbalimbali Afrika, Ulaya na Marekani.

Historia yake inamuonesha, licha ya
kuzaliwa Arusha, ule mji wetu wenye vivutio vingi vya kitalii, pia
amekulia katika nchi nyingi tofauti Afrika na nje ya bara hili, ambako
bila shaka amejifunza mila, utamaduni na desturi za watu wengi tofauti.
Nilimsikia kwa mara ya kwanza katika
muziki mwaka 2012 kama sikosei, katika wimbo wa Ommy Dimpoz wa Me and
You. Ukisikiliza vizuri kibao kile, unafahamu fika kuwa yule mdada
anaijua vizuri hii lugha iliyokuja kwa ndege, Kiingereza.
Kwa mara ya kwanza, nilimuona ‘live’ wiki chache zilizopita, alipotembelea chumba cha habari cha gazeti hili na kufanya mahojiano na kituo chetu cha televisheni mtandaoni, Global tv online. Kwa mazungumzo yake siku hiyo ni binti ambaye yupo vizuri kichwani, kwa maana anajitambua!
Siku chache baadaye, nikaona habari yake katika mtandao mmoja maarufu wa habari za muziki na mastaa wa Bongo, akisema kuwa staili yake ya kuvaa nguo fupi ni katika kulenga kutengeneza brand yake, kwani ana malengo nayo siku zijazo.

Mtazame hata katika video za nyimbo zake
nyingi ni mtu mwenye kupenda mavazi ya Kimagharibi, yale ambayo kitovu
siyo kiungo chenye tofauti na kiwiko cha mkono!
Well, kila mtu ana malengo yake na inapotokea hivyo kwa vijana kama Vee Money ni jambo la kujivunia kuwa katika umri huo, amelenga kuwa mtu f’lani siku zijazo. Si watu wengi wa umri wake wanafikiri kuwa akina nani siku zijazo zaidi ya kuyumba na upepo, leo wanataka kuwa kama John Magufuli, kesho kama Edward Lowassa keshokutwa kama Reginald Mengi na mtondogoo kama Beyonce!
Lakini kama msanii, kwa maoni yangu, suala la kuwekeza katika nguo fupi, haliendani na mila na desturi za Kitanzania, hasa kwa watoto wa kike. Nakumbuka, hata alipofika chumba cha Habari cha Global Publishers, alikuwa akikaa kwa shida kutokana na ufupi wa nguo aliyovaa.

Kama lengo ni dili za ‘mbele’ kama
wenyewe mnavyosema, nadhani ilikuwa ni busara kama angekaa kimya na hilo
kubakia moyoni mwake, lakini kuvaa nguo fupi mbele ya wazazi, kaka na
dada zako kwa sababu tu unalenga kitu f’lani mbele ya safari, siyo jambo
la kujivunia kwa binti wa Kitanzania.
Kitakachomfanya yeye kuwa brand ya watu
kuvutika naye, ni kazi yake, wala siyo muonekano wake. Tunawapigia
kelele wale wadada wa Bongo Muvi, siyo kwa sababu tunawaonea wivu na
muonekano wao mzuri wakiwa katika mavazi ya nusu utupu, bali kwa kuwa
hawalisaidii taifa katika kutengeneza maadili yanayotakiwa, ambayo ndiyo
kazi yao kubwa kama vioo vya jamii.
-GPL
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )