October 09 2015 kuna tukio lilitokea linalomhusisha kijana Benedicto Ngonyani ambaye alituhumiwa kusambaza ujumbe ambao ulichukuliwa kama ni uzushi na kinyume cha sheria ya makosa ya mtandao.
Ujumbe huo
ambao ulisambaa kwenye mitandao ya kijamii ulikuwa ukisema kwamba Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali Davis Mwamunyange amepewa sumu,
suala hili lilipelekea kijana huyo kukamatwa na kupelekwa rumande.
Ayo TV imezungumza na wakili wa Benedict Ngonyani, Edward Kikuri ambaye ameeleza kesi hiyo ilipofikia hadi sasa ………
>>>’kesi
imesimama kisutu kwa sababu jalada halipo, lipo Mahakama Kuu na sisi
mawakili wa upande wa utetezi hatujapata wito wowote wa kuendelea na
rufani hiyo isipokuwa mawakili wa serikali huwa wanaiambia mahakama
kwamba kesi ya rufani au ya kupinga kupewa rufani ipo tayari mahakama
kuu‘
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )