Hivi
karibuni yalitua madai kwenye meza ya gazeti hili yakieleza kuwa, eti
yule wifi nambari moja wa Zarinah Hassan ‘Zari’ anayefahamika kwa jina
la Esma Platnumz (pichani) ametimuliwa pale nyumbani kwa Mwanamuziki
Nasibu Abdul ‘Diamond’, Madale jijini Dar na sasa anaishi Tandale.
Chanzo chetu ambacho kiliomba jina lake lisiandikwe gazetini kilidai kuwa, baada ya Zari kutua Bongo kabla ya kwenda Ulaya, Esma alitakiwa kufungasha kila kilicho chake na kwenda kuishi kwenye ile nyumba ya familia iliyokuwa ikikarabatiwa pale Tandale.
Ili kupata ukweli wa madai ya kutimuliwa, paparazi wetu alimvutia waya Esma na alipopatikana alisema: “Nyie bwana, mimi ni wa kutimuliwa pale kwa Diamond? Huwa naishi pale na nikipenda ndiyo nakwenda Tandale lakini hayo mambo ya kwamba nimetimuliwa ili kumpisha Zari ajiachie na Diamond ni vijineno tu vya watu.”

“Nyie mbona mnapitwa na ubuyu? Esma katimuliwa pale kwa Diamond, sasa hivi anaishi kule Tandale kisa ni zile figisufigisu zilizokuwa zikitokea kati yake na Zari.
“Diamond ameona ili mzazi mwenzake awe na amani, anayeweza kuondolewa kwenye ule mjengo aondolewe ili amani itawale na kusiwepo manenomaneno,” kilidai chanzo hicho.Siku chanche baada ya ubuyu huo kunaswa, paparazzi wetu akiwa kwenye mishe zake alimuona Esma nje ya nyumba ya akina Diamond iliyopo Tandale huku akionekana kuwa, yupo maskani yake mapya.
Ili kupata ukweli wa madai ya kutimuliwa, paparazi wetu alimvutia waya Esma na alipopatikana alisema: “Nyie bwana, mimi ni wa kutimuliwa pale kwa Diamond? Huwa naishi pale na nikipenda ndiyo nakwenda Tandale lakini hayo mambo ya kwamba nimetimuliwa ili kumpisha Zari ajiachie na Diamond ni vijineno tu vya watu.”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )