Huko kwenye mitandao ya kijamii kumechafuka habari ya Ali kusign deal na Sony wengi wakiamini huo ndio utakuwa mwanya wa msanii huyo kutoboa kimataifa.. Jambo ambalo mashabiki wake wanashindwa kuelewa ni kuwa huo unaweza kuwa anguko la King Kiba badala ya kuwa neema..
Kwanza kabisa kitu ambacho hawakielewi ni kuwa Ali hajasaini na Sony Music Ent. BMG (ishu yake sio 'global deal') bali amesaini na Sony Music Africa ambayo ni subsidiary ya Sony Music Entertainment!! Kwa ninavyoelewa Sony Music Africa wana sambaza mziki na kumanage wanamuziki ndani ya Africa pekee.. Sasa eidha Ali hajui alichosaini au chumvi inaongezwa kunogesha habari..
Kingine watu wanaona hii ni kama Bahati Ali amepata wanachoshindwa kuelewa ni kwamba wasanii wakubwa Africa huwa wanakataa kusign na hizi kampuni zenye asili ya marekani na ulaya kutokana na kampuni hizi kushindwa kutimiza malengo na kutoelewa mazingira ya soko la mziki Africa! Kwa mfano wasanii wote ambao wamewahi kusign na Sony karibia wote walikuja kufa kimuziki kutokana na Sony kushindwa kuwa market kutokana na kutoelewa mziki wa Africa; mfano wasanii kama Nakaaya Sumari, Nneke Egbuna (Nigeria), Luncvile (SA), Nathan Ro (SA) wote hawa wamepotea kwenye mziki..
Mfano mwingine ni msanii D'banj ambaye aliondoka Mavins na kujiunga na label ya GodLife chini ya kanye west, mpaka sasa D'banj anasafiria jina lake tu lakini kimuziki ameshuka vibaya sana!! Kampuni za kimarekani hazina record ya kuwatoa wasanii wa kiafrika na hii inatokana na kutoelewa industry yetu na ndio maana Psquare walikataa mabilioni waliyotaka kupewa ili wasign Convict records..
Kingine kinachosemwa na watu ni kwamba hizi kampuni zina mambo mengine makubwa zaidi kwahiyo inakuwa nguvu kwao kuwa serious sana na mwanamuziki mmoja mmoja; kwa mfano kampuni mama ya Sony Music Africa (Sony Entertainment BMG) ina zaidi ya label 25 ndogo ndogo kama hii aliyosign kiba na ina wasanii karibia katika kila nnchi ya ulaya, Asia na Amerika ya kusini. Wana zaidi ya wasanii elfu moja wanaowasimamia so inakuwa ngumu kwao kutoa macho kwa msanii mmoja mmoja na ndio maana wasanii wengi wakubwa wa Africa wanakataa kusign chini yao wanaona ni afadhali watengeneze timu zao wenyewe za management ambazo macho yao na attention yote itakuwa kwao wao kama wasanii..
Anyways, let me just assume management ya Ali inafahamu vitu ambavyo mimi sivifahamu na wamefanya research ya kutosha kabla ya kusign na hatimaye watatuprove wrong wote ambao tuko sceptical about this deal.!!
Kama kijana mwenzangu namtakia kilala kheri na mafanikio katika safari yake mpya...
By The bold
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )