Jenerali Erdal Ozturk aliyekuwa kinara wa jaribio lililoshindikana la mapinduzi ya rais nchini Uturuki amekamatwa, huku viongozi wengine wa mapinduzi hayo, saba wakifanikiwa kutoroka na kukimbilia nchi jirani ya Uturuki kwa kutumia Helikopta.
Jenerali Erdal Ozturk (kulia) enzi akiwa kazini.
Hata hivyo viongozi hao waliokimbilia nchini Uturuki wakiwemo mameja wawili, makapteni watano na raia mmoja wamekamatwa nchini humo kwa kile kilichoripotiwa kuingia nchini humo bila kibali.Jenerali Erdal Ozturk aliyekuwa kamanda mkuu wa kikosi namba tatu tayari amekamatwa na kuwekwa mahabusu wakati akisubiri hatma yake na huenda akanyongwa ikiwa atapatikana na hatia hiyo.
Mapinduzi hayo yalishindikana baada ya wananchi wengi kujitokeza kumsapoti Rais Recep Erdogan, ambaye ametamka bayana kwamba wote waliohusika na jaribio hilo lililoshindikana watakabiliwa na adhabu ya kifo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )