Mwenyekiti wa Kitongoji cha Buyango, Gasper Joseph amesema wamelazimika kuita wananchi ili kuutambua mwili wa marehemu.
Amesema licha ya kiwiliwili kutelekezwa kwenye eneo la kichaka, kichwa cha marehemu huyo wa kiume hakikuwapo kwenye eneo hilo jambo ambalo alilosema limeleta hofu kwa wananchi.
“Nimeita watu na walikusanyika, hata hivyo walishindwa kuubaini mwili huo kwa kuwa kichwa chake hakikuonekana. Mwenyekiti wa Kijiji cha Rushwa alitoa taarifa polisi kwa ajili ya hatua zaidi ili turuhusiwe kuzika,” amesema Joseph.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )