Featured
Loading...

Chid Benz hakujuwa kama Raymond angeshirikishwa kwenye wimbo wake mpya

Rapper Chid Benz amedai kuwa hakujuwa kama Raymond angeshiriki kwenye wimbo wake mpya ‘Chuma’ japo alimsaidia kuutayarisha.
Chidi
Chidi Benz amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa vitu vingi vilivyokuwa kwenye wimbo huo amefanya mwenyewe lakini Raymond alikuwa anamsaidia baadhi ya vitu ndani ya wimbo huo kuvirekebisha mpaka alipomaliza.
Chid amedai baada ya kumaliza kurekodi wimbo huo, aliuachia uongozi wa WCB uamue cha kufanya.
Naye Raymond amesema, “Kwanza mimi nashukuru sana kwa sababu brother Chid Benz kitambo mimi namsikia.” Lakini pia aliongezea kuwa wakati Chid Benz anaachia wimbo wake wa kwanza mwaka 2005 yeye alikuwa darasa la nne.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top