Muigizaji Esha Buheti amefunguka kwa kusema kuwa heshima ya tasnia ya filamu imeanza kurudi katika hali yake ya kawaida baada ya kuyumbishwa na baadhi ya wadau.
Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Esha Buheti amesema tasnia ya filamu ilikuwa inayumbishwa na baadhi ya wasambazaji wa filamu.
“Kusema kweli hapo nyuma kulikuwa na tatazo la wasambazaji, lakini tayari naona hali imenza kukaa vizuri, wasambazaji wameongezeka. Kwa hiyo bila shaka naona mambo mazuri yakujua katika siku za usoni, watu wategemee mambo makubwa, na heshima ya tasnia ya filamu itarudi,” alisema Esha Buheti.
Pia muigizaji huyo amewataka mashabiki wake wa filamu kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio wa filamu yake mpya ambayo inatoka hivi karibuni.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )