Henry ameamua kuacha kazi ya kuendelea kukifundisha kikosi cha vijana cha Arsenal, baada ya kocha mkuu wa Arsenal Arsene Wenger kuamua kumwambia kuwa achague moja kama kufanya kazi ya ukocha ndani ya Arsenal au kuendelea na kazi ya uchambuzi wa soka katika kituo cha Sky Sports.
Baada ya kauli ya Wenger imemfanya Thierry Henry ameamua kuacha kazi Arsenal na kuendelea na kazi yake ya uchambuzi, kama utakuwa unakumbuka vizuri Henry aliwahi kuichezea Arsenal katika kipindi cha miaka zaidi ya 7 na baadae kwenda kucheza soka katika klabu ya New York Red Bulls ya Marekani.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )