Mchezaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Neymar amefunguka juu ya maamuzi ya Lionel Messi kutangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa.
Neymar amesema kuwa ni uamuzi mgumu sana aliofanya [Messi] kustaafu soka la kimataifa, lakini anatumai ana furaha.
Akiongea na gazeti la Marca la Hispania, Neymar amesema, “I respect his decisions, but football without Messi isn’t football, it’s hard to imagine it without him.”
“If you like football at all, then you can’t help but admire Messi and everything he’s achieved for Argentina and Barcelona,” aliongeza.
Aidha Neymar ameeleza kuwa hana wazo la kuondoka Barcelona akipinga tetesi zinazozidi kuenezwa kuwa hana furaha ndani ya timu hiyo huku ikielezwa kuwa anaweza akatua kwenye timu ya PSG
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )