Kila
siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za
Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account
yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza
kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya habari zilizoandikwa kwenye magazeti ni hii kwenye gazeti la Jambo Leo yenye kichwa cha habari ‘Jambazi aliyetoroka Mwanza aibua hofu’
Gazeti
la Majira limeripoti kuwa baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wamekumbwa
na hofu kuhusu usalama wa maisha yao baada ya mmoja kati ya majambazi
aliyehusika na mauaji ya waumini watatu katika msikiti wa Rahman na
kufanya uhalifu katika maduka ya M-Pesa, Tigo-Pesa, Airtel Money, Hamis
Juma (38) kutoroka chini ya ulinzi wa askari Polisi.
Tukio
hilo ambalo lilitokea Julai 3 mwaka huu, saa 2:00 usiku katika eneo la
mlima Kiloreli Nyasaka, Manispaa ya Ilemela, limeibua hofu kwa wakazi wa
jiji hilo kutokana na mfululizo wa matukio ya uhalifu wakidai
kushangazwa na jambazi huyo kuwatoroka Polisi.
Baadhi
ya wananchi waliozungumza na gazeti hilo kwa masharti ya kutotajwa
majina yao gazetini, walihoji askari wa idara ya upelelezi walijiamini
vipi kwenda na jambazi huyo mafichoni kwa wenzake bila kuwa na ulinzi wa
kutosha kumfunga pingu za miguu, mikono.
”Tulitilia
mashaka tukio hili kutokana na matukio yanayoendelea kutokea, tumezoea
kuona polisi wakiwafunga pingu za mikono au miguu watuhumiwa mbalimbali
wanaokamata hata kama hana madhara, iweje jambazi asifungwe pingu”
”Jambazi
aliyetoroka ameshiriki tukio kubwa la kuuawa watu wasio na hatia,
watuhumiwa wa matukio ya kigaidi hupelekwa na mahakamani chini ya ulinzi
mkali wa polisi wenye silaha nzito’‘
Akijibu
tuhuma hizo, kamanda wa Polisi mkoani humo, Ahmed Msangi alisema tukio
hilo lilikua la ghafla, polisi ni binadamu, wakiwa njiani kwenda
mafichoni ghafla majambazi walianza kuwashambulia ikabidi wachukue
tahadhari ili kujihami na mashambulizi kwa kujibizana nao risasi ndipo
jambazi huyo akatorokaTupe Maoni Yako( Matusi Hapana )