Mwenyekiti wa Kamati ya maadili ya TFF, Wilson Ogunde amesema kuwa walikuja kukutana wakiwa na mashauri matatu ambapo shauri la kwanza na la pili limeweza kusikilizwa na mashahidi kupewa nafasi ya kujitetea lakini katika shauri la Jerry Muro tumeambiwa yupo ila amesema kuwa hataweza kuingia ndani kwa sababu barua haijamuelekeza ni wapi anatakiwa kwenda pia hakukuwa na uambatanisho wa mashtaka dhidi yake ila tumepewa taarifa kuwa ametumiwa na Email pia Julai 01 inawezekana akawa hajaisoma na kwa mamlaka kabisa tumejadiliana tumeamua kulirudisha suala hili kwenye sekretarieti ya TFF kama watahitaji kuendelea basi wamuandikie barua ya wito uliojitosheleza.
Amesema, Muro ana haki ya kujitetea na kuleta ushahidi wake na katika kusikiliza shauri lazima.upande wa mshtakiwa aridhike na mashtaka yake na kama kuna mapungufu anaweza kuomba kusogezwa mbele na katika hali ya kujitetea kwa upande wake amesema kuwa hawezi kuingia kwenye hiyo kamati kwani hakutambua kama anaitwa huko pili ajajiandaa kisaikolojia na hajaambatana na wakili wake.
Naye baada ya shauri dhidi yake kutupiliwa mbali, Muro amesema kuwa aliyeandika barua ile alikurupuka na zaidi kama angekubali kuingia kwenye kamati ile basi haki isingetendeka na zaidi wametuma taarifa ya kwanza ambayo ni Juni 29, wakatuma Email Julai 01 na hajaitumia kwa muda mrefu. Kwahiyo kama watanihitaji waandike shauri lingine sio kutaka kumfanyia mtu njama ilimradi asijihusishe na masuala ya mpira tena.
Hii mara ya tatu kwa Muro kuitwa ila mara zote amekuwa akishinda kesi hizo za maadili
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )