Featured
Loading...

Muimbaji wa Tanzania aishiye Merakani, Erica Lulakwa atoa ujumbe huu kuhusiana na ajali za mabasi

Ajali mbaya iliyohusisha mabasi mawili ya kampuni moja, City Boys Jumatatu hii ilisababisha vifo vya takriban watu 30. Mabasi hayo yaligongana uso kwa uso katika Kijiji cha Maweni, Manyoni mkoani Singida. Muimbaji wa Tanzania aishiye Marekani, Erica Lulakwa anaamini ajali kama hizo hutokea kutokana na uzembe wa madereva ambao wakati mwingine abiria huuendekeza pia. 12565468_1030607993644648_3499463625021897197_n
“Nikitua Tanzania Dar es Salaam, Ni lazima nipande basi kuelekea Singida masaa 9-10 barabarani,” ameandika kwenye Facebook.
“Kwa Bahati nzuri basi ninazopanda huwa ma dereva wanaoelewa nini maaadili ya kazi zao. Mara 2 hivi nilikosa nafasi Katika gari hizi, nikielekea Katika mazishi ya dada yangu mpendwa, Mwaka 2012. Nilipanda gari ambalo sikuwa nimezoea kupanda. Dereva aliendasha Kwa Kasi sanaaaaa. Abiria wakawa wanashabikia dereva kanyaga twende. Wachache tukawa tunamwambia aendeshe Kwa speed inayoonyeshwa barabarani. Hakutuelewa. Nikaamka Na kumfuata nikamwambia dereva endesha Kwa speed iliyopangwa la sivyo simamisha gari wanaotaka kushuka washuke halafu tutaonana kituoni police Na fedha za abiria utarudisha. Akaniangalia lakini akapunguza mwendo.,” ameongeza.
“Maana yangu ninini, tu ache ushabiki watanzania tukiona dereva anafanya sivyo. Mfuateni Katika kiti chake Na mmuonye asi endelee kuhatarisha maisha ya mtanzania. Tuache woga wakati wa Hali hatarishi. Waonyesheni madereva kwamba mnajali uhai wenu. La sivyo abiria wataendelea kupoteza maisha Na baadhi ya watu wataendelea kula lama Tu bila vitendo Na haki tunayosisi wananchi (abiria). Inavyosemekana Hii ajali imetokea Kwa mzaha tu. Poleni wote mliopatwa Na mkasi Huu.”

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top