Mchezaji wa zamani wa timu ya Barcelona, Hristo Stoichkov amedai kuwa Ronaldo anaweza akatwaa tuzo ya Ballon d’Or.
Hristo Stoichkov ambaye alifanikiwa kuichezea timu a Barcelona mara mbili tofauti kwa miaka saba na kucheza jumla ya mechi 175 na kufunga magoli 84, ameiambia radio ya Cadena Cope ya Hispania kuwa kutokana na umbile la Ronaldo anaweza akapewa tuzo ya Ballon d’Or.
“Griezmann is blowing everyone away and playing some spectacular football. But they’ll probably give it to Cristiano Ronaldo again for being guapo [handsome]!,” alisema Stoichkov.
Aidha Stoichkov ameongeza kuwa Gareth Bale atakuwa miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo hiyo iwapo Wales itatinga fainali ya michuano ya Uero inayoendelea huko nchini Ufaransa.
Stoichkov amefanikiwa kuchukua tuzo hiyo ya Ballon d’Or mara moja nao ni mwaka 1994 akiwa na timu ya Barcelona.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )