Featured
Loading...

Nchi 5 ambazo Askari hawaruhusiwi kubeba silaha za moto kwenye doria


Mauaji ya raia imekua topic kubwa kwenye media mbalimbali duniani kwa siku chache zilizopita na hiyo ni baada ya Polisi ‘Wazungu’ kuua Wamarekani weusi huku mauaji hayo yakinaswa na camera za simu za mashuhuda.
Vifo hivyo vilipelekea mpaka Mwanajeshi mmoja wa zamani mwenye utaalamu wa kulenga shabaha kwenye mji wa Dallas Marekani, kujitoa muhanga na kuua askari watano na kujeruhi wengine kadhaa kwa hasira za kulipiza kisasi cha Weusi wenzake kuwawa.
Marekani 3
Inawezekana visa vyote hivi visingetokea kama Askari wa Marekani wasingekua na silaha za moto na badala yake wakimkamata Muhalifu wanamfunga pingu na kumpeleka kituoni ila kwasababu wote walifanya mauaji hayo kwa kutumia bastola, visa vya kulipiza visasi ndio vikaibuka kwenye miji zaidi ya mitatu baada ya video zilizonaswa kuonyesha uonevu.
Kuna nchi ambazo zinaweza kuepuka balaa kama hilo sababu askari wao hawaruhusiwi kisheria kuwa na silaha za moto kwenye doria ambapo nchi hizo ni Ireland, Norway, Iceland, New Zealand na Britain.
Askari wa hizo nchi tano huruhusiwa kubeba silaha za moto pale tu kunapokua na matukio maalumu au kwenye ishu nzitonzito, pia kwa upande wa Marekani mpaka sasa ni zaidi ya watu 512 wameuwawa na Polisi toka mwaka 2016 uanze wakati mwaka 2015 ni watu 990.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top