Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akiwaapisha makamishna wa Jeshi la Polisi waliopandishwa vyeo na kuongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba mabilioni hayo yalitolewa kwa siku moja lakini hadi leo hakuna hata sare moja ya iliyonuuliwa.
Ameshangazwa na jeshi hilo kutoa kiasi cha fedha kinachokadiriwa kuwa kati ya shilingi bilioni 40 hadi 60 kwa ajili ya sare za polisi ambazo hadi leo hakuna hata moja iliyonunuliwa na wakati huohuo jeshi hilo likikosa shilingi bilioni 4 tu za kukomboa magari yao zaidi ya 70 yanayoshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) huko bandarini.
Aidha, Rais Magufuli ameagiza uchunguzi ufanyike na wahusika wafikishwe mbele ya haki ila angalau hata nusu ya fedha hizo ziweze kurudishwa zikalipie magari ya polisi yaweze kutoka bandarini maramoja.
Amelitaka pia Jeshi la Polisi kuachana na utaratibu wa kuwa na watumishi ambao ni raia wa kawaida na badala yake polisi wenyewe ndio washike nafasi hizo kulingana na taaluma husika na kushangazwa na taarifa kuwa Mhasibu Mkuu wa Polisi aliyetumbuliwa hivi karibuni kwa tuhuma za ubadhirifu alikuwa raia wa kawaida na sio polisi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )