Jana July 29 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alianza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo alizungumza na wananchi wa Manyoni Singida na kutoa onyo kwa watakaoanzisha maandamano.
"Wasije wakanijaribu mimi ni tofauti sana, na kama wapo watu wanawatumia wakawaeleze vizuri mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa, siasa nzuri wananchi wetu washibe, wapate madawa, nataka hao wanaotetea maandamano watangulie wao halafu wataona cha mtemakuni"- Alisema Rais Magufuli
Hapa chini ni sauti ya Rais Magufuli sehemu ya kwanza na ya pili. Msikilize.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )