Featured
Loading...

Ryan Giggs Kuondoka Man United....


Ryan Giggs amefikisha kikomo cha muda wake wa kuhudumu katika klabu ya Manchester United baada ya kukubali kuondoka kupitia makubaliano.

United inatarajiwa kutoa taarifa rasmi katika siku chache zijazo kuhusu hatua hiyo.

Giggs mwenye umri wa miaka 42,alikuwa amesalia na mwaka mmoja katika kandarasi yake kama naibu meneja, lakini mkufunzi Jose Mourinho anataka nafasi yake ichukuliwe na rafikiye Rui Faria.

Huku akishindwa kuafikia makubaliano ya kuchukua wadhfa mwengine katika klabu hiyo ya ligi kuu ya Uingereza,Giggs ambaye aliichezea Man United takriban mara 963 amekubali kuondoka....

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top