Featured
Loading...

Sallam Atoa Sababu ya Kuchelewa Kutoka kwa Video ya Wimbo wa Diamond na P-Square


Diamond ana kesi kwa mashabiki wake. Ijumaa na Jumamosi hii wamekuwa wakisubiri kwa hamu video ya wimbo wake aliowashirikisha P-Square ambayo aliahidi ingetoka jana, lakini hadi sasa kimya!!

Wengi wameonesha kukusa uvumilivu na wameanza kuelezea kusikitishwa kwao kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Lakini tumeongea na uongozi wake kutaka kujua nini sababu za kuchelewa kutoka kwa video hiyo, na umesema kuwa kuna vitu vichache vimechelewesha na kwamba mashabiki wasiwe na shaka kwasababu kiu yao itakatwa.

“Kuna vitu vinachelewesha ila tupo katika final touches,” meneja wa Diamond, Sallam ameiambia Bongo5.

“Ukiwapa kitu kibaya watalalamika ni bora wafanye subira wapate kizuri zaidi,” ameongeza.

Video ya wimbo huo ilifanyika nchini Afrika Kusini na utakuwa wimbo wa kwanza P-Square wanasikika wakiwa pamoja tangu kundi lao kudaiwa kuvunjika.

Ijumaa hii Diamond alipost kwenye Instagram picha ya mwanae Tiffah mwenye umri wa miezi 11 sasa na kuandika: On the LONG conversation with my Miss World before Making a History.”

Ujumbe huo uliwapa matumaini mashabiki wake kuwa muda wa kuiona video hiyo umekaribia.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top