Qandeel Baloch, aliyekuwa miongoni mwa mastaa wa mitandao ya kijamii nchini Pakistan, ameuawa na kaka yake katika mji wa Multan uliopo kwenye jimbo la Punjab. Alidai amemuua dada yake kwa heshima.
Polisi wamedai kuwa Baloch aliuawa na kaka yake kwenye nyumba ya familia yao baada ya kuchukizwa kwa muda mrefu na picha ambazo dada yake alikuwa akizipost mtandaoni.
Baada ya kutekeleza mauaji hayo kaka yake alikimbia japo baadaye alikamatwa na polisi na kukiri kuhusika mbele ya waandishi wa habari.
Msichana huyo alikuwa akiweka picha za kawaida ambazo mastaa wengine duniani hupenda kuziweka kuonesha urembo wao.
Hata hivyo kwa maisha ya Pakistan na sheria zake, Baloch alionekana kuwa ‘controversial’ japo alipendwa sana.
Alikuwa na karibu wafuasi 750,000 kwenye mtandao wa Facebook ambako video zake zilikuwa maarufu na kuzalisha mijadala nchini humo.
Alijipatia umaarufu zaidi nchini humo baada ya kuahidi kuwa angevua nguo online kama timu ya Pakistan ingeshinda kwenye mchezo wa cricket dhidi ya mahasimu wao India.
Baloch alitengeneza pia vichwa vya habari baada ya kupost selfie kwenye Instagram akiwa na Mufti Abdul Qavi, moja ya viongozi wa dini nchini humo na kupelekea kusimamishwa wadhifa huo.
Kaka yake alidai kuwa skendo zake ndizo zilimfanya achukue uamuzi wa kumuua.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )