Featured
Loading...

Staa wa Real Madrid amegoma kujiunga na Man United ya Jose Mourinho


July 21 2016 bado headlines za magazeti mengi ya michezo barani Ulaya yameamka na headlines za usajili, katika kipindi hiki ni kawaida kusikia mchezaji fulani akihitajika na timu fulani, sasa leo July 21 2016 beki wa kati wa Real Madrid Raphael Varane ameingia kwenye headlines baada ya kugoma kujiunga na Man United.
varanexx
Stori za Raphael Varane kugoma kujiunga na Man United inayofundishwa na Jose Mourinho kocha ambaye amewahi kumfundisha wakati akiwa Real Madrid, zimeandikwa katika gazeti la Marca la Hispania katika ukurasa wa mbele, Marca wanasema kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane ndio anatajwa kuchangia mchezaji huyo kugoma kwenda Man United.
varaneno
Jose Mourinho ambaye ameshawasajili Eric Bailly kutoka Villarreal, Henrikh Mkhitaryan kutoka Borussia Dortmund na Zlatan Ibrahimovic, anatajwa kuwa alikuwa na mpango wa kumsajili Varane ili kuimarisha nafasi ya beki wa kati, lakini sasa atalazimika kutafuta mbadala wake sehemu nyingine.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top