Usiku wa July 28 klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji inayochezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta ilishuka tena dimbani kucheza mchezo wake wa kwanza wa round ya pili wa kuwania kucheza hatua ya makndi ya Kombe la UEFA Europa League dhidi ya Cork City ya Ireland.
Mchezo wa kwanza wa round ya pili ya Europa League KRC Genk wameanzia katika uwanja wao wa nyumbani wa Cristal Arena
wenye uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya 24000 na kufanikiwa kuibuka
na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na mjamaica Leon Bailey dakika ya 31 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa mshambuliaji wa Kigiriki Nicolaos Karelis.
Hata hivyo licha ya KRC Genk kupata ushindi huo wakiwa pamoja na nyota wao kutoka Tanzania Mbwana Samatta, bado wana wakati mgumu katika mchezo wa marudiano watakaocheza August 4 Ireland, kwani watakuwa wanahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ile ili waweze kusonga mbele katika hatua inayofuata na kuitoa Cork City.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri KRC Genk wamekutana na Cork City, baada ya kuitoa Buducnost ya Montenegro kwa mikwaju ya penati 4-2, baada ya mechi yao ya mwisho kumalizika kwa Buducnost
kuibuka na ushindi wa goli 2-0 ila kutokana na kuwa na aggregate ya 2-2
walilazimika kucheza dakika 120 na baadae mchezo ukaamuliwa kwa mikwaju
ya penatiTupe Maoni Yako( Matusi Hapana )