Featured
Loading...

Vyeti ni gonjwa kwa watumishi, wengi wahaha kutangaza vimepotea



Wakati serikali ikiendelea kuhakikisha vyeti kubaini watumishi wasiokuwa na sifa, watu wengi wamejitokeza kutangaza kupotelewa na vyeti magazetini

Katika kipindi ambacho taasisi mbalimbali zinaendelea na zoezi hilo imebainika kuwa siku za nyuma kulikuwa na matangazo ya aina tofauti lakini kwa juzi kumetokea mtiririko wa watu kutangaza kupotelewa na vyeti hali isiyo ya kawaida kwa taifa.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Ufundi , Profesa Joyce Ndalichako alisema juzi kuwa serikali itafanya uhakiki wa vyeti katika vyuo na sehemu za kazi.

Naye Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)Godius Kahyarara juzi alitoa waraka akisema wafanyakazi watakaoshindwa kuwasilisha vyeti vyao halisi hawatalipwa mishahara.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top