Featured
Loading...

Wema hana haja ya kuwa na meneja – Mama Wema

Mama yake Wema Sepetu, Miriam Sepetu amesema huu ni wakati wa mwanae kujisimamia mwenyewe katika kazi zake.
wema
Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Mama Wema amesema umri aliokuwa nao mwanae kwa sasa anaweza kufanya kazi zake bila meneja.
“Mwanangu sasa hivi amekuwa sana, na siku zote nimekuwa nikimpigia kelele swala kufanya kazi bila kuwa na mameneja,” alisema Mama Wema. “Mimi naona wanamchanya tu, kama akiwa na wazo anakuja kwangu anampa ushauri na mambo yanaenda, huu ni wakati wa Wema kusimama mwenyewe, hana haja ya kuwa na meneja,”
Pia Mama Wema alimsifia mwanae kwa kuandaa show ya ‘The Black Tie’ iliyofanyika weekend iliyopita katika ukumbi wa King Solomon jijini Dar es salaam.
Katika hatua nyingine Mama Wema alikataa kumzungumzia Martin Kadinda ambaye ndiye aliyekuwa meneja wa mwanae.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top