Kutokana na maombi ya klabu nyingi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutaka kuandaa wachezaji kwa ajili ya Ligi Kuu msimu unaoanza sasa, umemlazimu Kocha Mkuu timu ya Mpira Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa kuahirisha kambi iliyokuwa ianze Jumatatu Agosti mosi, mwaka huu, imefahamika.
Wachezaji ambao Mkwasa amewaita wanatoka kwenye klabu mbalimbali na ambazo zinaongoza kutoa nyota wengi ni Simba SC, Young Africans SC, Azam FC na Mtibwa Sugar FC.
Hivyo basi, Mkwasa sasa atakuwa anafuatilia mwenendo wa nyota 24 aliowaita kwenye michezo mbalimbali ya kirafiki wa klabu hizo inayofanyika kabla ya kuanza Ligi Kuu Tanzania Bara (Pre-season matches) na michezo ya raundi ya kwanza na pili ya Ligi Kuu kabla ya kukiita tena kikosi hicho kwa ajili ya safari ya kwenda Nigeria.
Taifa Stars ina mchezo na jijini Lagos, Nigeria Septemba 2, 2016 ambao ni wa kukamilisha ratiba katika kundi G baada ya Misri kusonga mbele wakati Chad kujitoa. Wachezaji ambao Mkwasa aliwaita mapema wiki hii ni:
Makipa:
Deogratius Munishi
Aishi Manula
Benny Kakolanya
Mebeki:
Kelvin Yondani
Aggrey Morris
Oscar Joshua
Mohamed Husein ‘Tshabalala’
Juma Abdul
Erasto Nyoni
Viungo:
Himid Mao
Mohamed Ibrahim
Shiza Kichuya
Jonas Mkude
Ibrahim Jeba
Mwinyi Kazimoto
Farid Mussa
Juma Mahadhi
Hassan Kabunda
Washambuliaji:
Simon Msuva
Joseph Mahundi
Jamal Mnyate
Ibrahim Ajib
John Bocco
Jeremia Juma
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )