Na Maelezo-Zanzibar
Chama cha Wakulima (AFP) kimelaani
vikali dhidi ya hujuma zilizoandaliwa kufaywa na Umoja wa Wananchi
UKAWA ifikapo tarehe 1mwezi ujao.
Akizungumza na Waandishi wa Habari
Mwenyekiti wa Chama hicho Said Soud Said katika Ukumbi wa Sanaa uliopo
Rahaleo Zanzibar amesema hujma hizo zilizoandaliwa na UKAWA za kufanya
maandamano makubwa ya kupinga Serikali iliopo madarakani zilizopangwa
nchi nzima zina lengo la kuvuruga amani nchini.
Amesema Jeshi la Polisi na
Wananchi kwa ujumla wametakiwa kuwa macho kutokana na kauli zinazotolewa
na baadhi ya viongozi wa siasa za kutaka kuchafua kwa makusudi na
kuipeleka nchi katika vurugu jambo ambalo litasababisha kuwepo vitendo
vibaya ikiwemo ubakaji na mauaji.
Aidha amesema Zanzibar haiwezi
kuvumilia kuingia katika vurugu hivyo Wananchi wasikubali kushawishiwa
na Wanasiasa wasiopenda maendeleo wanaotaka kuvuruga amani iliopo.
“Vijana msikubali kushawishiwa na
Wanasiasa wamejitokeza kwa ajili ya biashara hivyo natoa indhari hii kwa
kuwatahadharisha wazanzibari wenzangu kuachana na hujuma hiyo
inayoandaliwa,”Alisema Said Soud.
Hata hivyo amewaasa Vijana
kutokubali kushawishiwa na Wanasiasa kushiriki katika vurugu na badala
yake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika shughuli za kiuchumi na
maendeleo kwa lengo la kujikimu kimaisha.
Akizungumzia suala la amani na
utulivu Pemba Mwenyekiti huyo amefahamisha kuwa hali sasa ni
yakuridhisha kutokana na kupungua kwa kasi vitendo vya hujumaVisiwani
humo na.
“Jeshi la polisi kwa kushirikiana
na Serikali wamesaidia kwa kiasi kikubwa na kuwadhibiti wale wote
walioshiriki kufanya vitendo hivyo kwa kuchukuliwa hatua za kisheria,”
ameeleza Mwenyekiti huyo .
Sambamba na hayo Mwenyekiti huyo
ameipongeza Serikali iliopo madarakani kwa kuchukuwa hatua nzuri ya
kuimarisha Mji wa Zanzibar pamoja na Wafanya Biashara wa Darajani kwa
kuitikia agizo lililotolewa na Serikali la kuhama katika maeneo yao ya
kufanyia biashara na kuwataka kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki
ujenzi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )