"Siasa bwana wakati mwengine hovyo kabisa.
Eti Leo #JULIUSMTATIRO aliyechukuliwa na #Lipumba baada ya kuhitimu UDSM na Hekaheka za serikali ya wanafunzi DARUSO na kutelekezwa na Mnyika na Chadema anamwita #LIPUMBA msaliti!
..Duh kweli shikamoo Siasa,
Lipumba huyu huyu aliyempa Ukurugenzi wa sheria na haki za Binaadamu cheo kilichokuwa kikishikiliwa na Mbarala Maharagande Leo amemsaliti aliyemteua na kumpa mshahara kama njia ya kuwatia moyo vijana waliokuwa vyuoni wakifanya harakati.
Yaani #LIPUMBA aliyempa #MTATIRO unaibu Katibu Mkuu wa CUF from nowhere akimtosa #WILFREDLWAKATARE na kumpa muhitimu wa chuo kama chachu ya kuwatia vijana wengine Siasa bila kuwa na uzoefu wowote katika Siasa Leo amegeuka MSALITI mbele yake? ...
Kweli ukiwa unafanya Siasa uwe na ngozi ngumu aisee.
Ndio mana siasa inahusianishwa na uongo uongo na maneno mengi
Ukianza kuongea saaana unasmbiwa usilete siasa hapa. Ukiwa kigeugeu unaambiwa usilete siasa hapa.
Na Ndio mana naelewa Sasa kwanini #Mtatiro aliweza kuandika makala tuliyoipenda Sana ya #NJAAMPAKAmakanisani akiwalaumu viongozi wa Dini wanaopokea pesa za Lowassa lakini baadae akasimama kidete kumnadi huyo huyo Lowassa.
Nazidi kuelewa aisee. Siasa haihitaji uwe mkweli, ni kuongopa tu mwanzo mwisho ukisema ukweli inakula kwako.
Ni kama yule aliyewashauri watu wa Arusha wamzomee Lowassa kwa sababu ni Fisadi lakini alipohamia Chama chake akasimama kumnadi.
Ama yule mchungaji aliyesema "atakayemuunga mkono Lowassa akapimwe akili "...miezi michache baadae akawa mpiga debe wake Mkuu na fulana zenye picha yake akavaa.
Mwishowe watu wenye akili timamu watawadhalau wanasiasa kwa Unafiki wa namna hii.
Ndimi"
Habib Mchange
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )