Taifa la Nigeria jana liliingia
katika historia mpya baada ya kushuhudiwa chama cha upinzani kikishinda katika
uchaguzi mkuu wa nchi hiyo pale Jenarali Muhammadou Buhari wa chama pinzani cha
All Progressive Congress (APC) alipomshinda mpinzani wake aliekuwa rais wa nchi
hiyo na kilichokuwa chama tawala cha People's Democratic Party (PDP) Goodluck Jonathan
Rais
aliyekuwa madarakani Goodluck Jonathan
amesalia akijutia maamuzi yake baada ya raia wa taifa hilo kubwa zaidi Afrika
kiuchumi kumpigia kura mpinzani wake mkuu Muhammadu Buhari .
Haya hapa ni mambo makuu
5 ambayo yanaelezea kwanini raia wa Nigeria walimng'oa Goodluck
Jonathan madarakani
. 1: Haikuwa
rahisi kuiba kura
Katika
Uchaguzi uliopita wa mwaka wa 2007
,tuhuma za wizi wa kura za urais ziliibuka huku wadadisi na wachunguzi wakisema waziwazikuwa kura hazikuwa za huru
wala haki.
Ripoti ya wachunguzi katika uchaguzi wa mwaka wa 2011 ilisema kuwa
haukuwa wa uhuru japo ilisema kuwa idadi ya wizi ilikuwa imepungua mno.
Kufuatia ripoti hiyo tume huru ya uchaguzi nchini humo
ilijiandaa na kuziba mianya iliyokuwa imebainika.
Tume hiyo ilinunua mashine za kuwasajili wapiga kura kwa njia ya
kielektroniki na ving'amuzi vilivyotumika kubaini data ya mpiga kura.
Chama cha rais Goodluck Jonathan People's Democratic Party (PDP)
kilikuwa kimepoteza ufuasi mkubwa katika majimbo yaliyokuwa ngome yake.
2 Boko Haram
Uchaguzi
huo umetangazwa huku raia wengi wa Nigeria wakikabiliwa na changamoto ya
usalama wao haswa wakiwa mijini.
Hii inafwatia tishio la kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Boko
Haram ambao walikuwa wanaonekana ni kama wameishinda maarifa vyombo vya usalama
vya nchi hiyo
Boko Haram iliwaua zaidi ya watu elfu 20 na kuwalazimisha
wenyeji zaidi ya milioni tatu kutoroka makwao.
Rais Jonathan hakuwa na jibu dhidi yao na alionekana mnyonge hadi
majuzi majeshi ya muungano wa mataifa jirani yaliposhirikiana na jeshi la
Nigeria na kuwavamia wanamgambo hao wa kiislamu.
. 3 Muungano wa Upinzani
Chama
cha PDP kiliundwa kwa muungano wa viongozi kutoka matabaka ya kaskazini na
vilevile kusini mwa taifa hilo.
Hata hivyo kufuatia udhaifu wa rais Jonathan viongozi wengi waliokuwa
nguzo ya umoja huo walitawanyika.
Muungano wa viongozi wa upinzani chini ya nembo ya chama cha All
Progressives Congress (APC)kuliwasaidia kukusanya kura zote katika kapu moja.
4 Uchumi mkubwa
zaidi Afrika
Ijapokuwa
Nigeria inasifika kuwa taifa kubwa zaidi barani Afrika kiuchumi ,ukiwauliza
raia wa Nigeria iwapo wamenufaika kwa njia yeyote ile watakuambia kuwa
hawajanufaika kwa hali yeyote ile.
Takriban nusu ya raia wa nigeria wanaishi kwa hali duni ya
uchochole na umaskini.
Wengi wao wanalaumu ufisadi wa viongozi na ubadhirifu wa mali ya
umma.
Uchumi wa Nigeria umekuwa kwa kiwango cha asilimia 5% kwa mwaka
kutokana na mauzo ya mafuta lakini raia wengi hawakutaka kuendelea na utawala
wa Goodluck.
Takwimu
zinaonyesha kuwa kila watu 10 wanaohitimu chuo kikuu nchini Nigeria 6 kati yao
wanakuwa hawana ajira
5 Ni wakati wa Mabadiliko
Wafuasi
wa chama cha upinzani APC walichagua kibwagizo chao kikuu kuwa ''Mabadiliko''.
Na huenda wanigeria hawakuwa wanataka kuendelea na hali
ilivyokuwa wakati huu.
PDP imekuwa madarakani tangu mwaka wa 1999, utawala wa kiimla ulipomalizika.
Mwaka huu 2015 Wapiga kura wameamua kumchagua kiongozi
atakayekuwa na msimamo thabiti na uwezo wa kukabiliana na matatizo mengi
yanayowasakama
Hata hivyo kinachosubiriwa na wengi ni kuona iwapo rais Buhari
ataleta mabadiliko kweli alivyowaagiza wapiga kura.Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )