 |
|
Mapema wiki
hii katika kijiji cha Oshindi nchini Nigeria wananchi walishuhudia sinema ya
bure ambapo kamera zao zilikuwa macho yao na simu zao pale ndege aliyekuwa
anapaa angani ghafla alianguka chini baada ya kudandia nyaya za umeme na
kugeuka mwanamke.
Kitendo
hicho kiliwaacha wananchi vinywa wazi wasijue la kufanya huku wakibaki kupiga
picha kwa kutumia simu zao za mikononi.
|

 |
|
Mwanamke
huyo alionekana kuchubuka na kuwa na vidonda katika mwili wake hali iliyo kuwa
inahuzunisha huku akiwa haongei (bubu) .
Wananchi hao
walimuuliza maswali mengi wakitaka kujua imekuaje hadi akageuka binadamu wakati
yeye alikuwa ndege anapaa juu.
Mama huyo
aliwajibu kuwa alikuwa anaenda kumtazama binti yake aliyekuwa amejifungua muda
mchache.
Habari
zinasema kuwa mwanamke huyo alikuwa mchawi na binti yake alikuwa anafanya sala
wakati yule mama alikuwa anapaa.
Inaelezwa
kuwa wakati sala inaendelea ndipo mwanamama huyo aliyekuwa amejibadilisha na
kuwa ndege akageuka binadamu.
Taarifa
zinaarifu kuwa binti yake alikuwa kila akijifungua mtoto anafariki papo hapo.
|
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )