Featured
Loading...

Majibu ya Sober House kuhusu maendeleo ya msanii Ray C…..


Usiku wa June 16 2016 kuamkia June 17 kuna video ya mwimbaji wa longtime Bongoflevani Rehema Chalamila au Ray C ilisambaa mitandaoni akiwa anachukuliwa na gari la Polisi Kinondoni Dar es salaam ambapo baadae ilikuja kugundulika alipelekwa Hospitali.

Kesho yake mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba aliongea na Amplifaya ya CloudsFM pamoja na millardayo.com na kuthibitisha kwamba mwimbaji huyu amekubali mwenyewe kwa hiari yake na kupelekwa kwenye nyumba ya matibabu ya kuachana na dawa za kulevya huko Bagamoyo Pwani.

Sasa leo Agosti 6, 2016 tumepata taarifa nyingine kwamba staa huyo kahamishwa kutoka Sober House ya Bagamoyo  na kuhamishiwa Sober House ya wanawake tu walioathirika na madawa ya kulevya iliyopo Kigamboni.

Akizungumza na millardayo.com & Ayo TV mmiliki wa kituo hicho Nuru kayaongea haya..
Mimi naitwa Nuru ni mmiliki wa Sober House ya wanawake tu iliyopo Kigambo juzi tulipata ugeni kutoka kwa Msanii Ray C alikuja kuomba matibabu kwasasa yuko anaendelea vizuri na amekubaliana na hali yake’- Nuru

‘Tumempokea vizuri na yeye mwenyewe amefarijika sana kiufupi tu mashabiki wake wamuombee dua sana na mpaka sasa hivi afya yake inaendelea vizuri’- Nuru

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top