Alisema vijana wake wapo kazini kuhakikisha wanampata ndani ya saa 24 kama walivyoagizwa hapo jana.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla la kumtafuta baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika jengo hilo na kukuta huduma zinaendelea.
Akiwa katika jengo hilo akikagua ndani mara baada ya kupata kibali cha Polisi cha kufanya upekuzi, wateja wa Dk Mwaka walikuwa wanaendelea kuingia kufuata huduma ya matibabu huku wengi wao wakiwa kina mama.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )