Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju aonya vyama vya siasa kutumia maneno yanayovunja amani na usalama wa nchi.
Masaju
ambaye amezungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es
salaam leo, ametolea mfano Oparesheni UKUTA iliyotangazwa kufanywa na
CHADEMA na kusema kuwa ina maneno ya kijeshi yanayotumiwa kwenye
shughuli za kihalifu.
Amesema
neno UDIKTETA siyo sahihi kwa kuwa nchini Tanzania hakuna udikteta kwa
kuwa serikali inafanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria na nchi
inaendeshwa kwa kuzingatia mgawanyo wa madaraka wa katika miimili yote
mitatu ya dola.
“UKUTA
lengo lake ni nini, ni sawa na kuwatenganisha wananchi na serikali yao”
Amesema Masaju na kuwataka wananchi kutambua kuwa Septemba Mosi ni siku
ya Majeshi nchini huku akishangazwa na CHADEMA kuchagua siku hiyo
kuzindua kampeni yao aliyodai kuwa ina lengo la kuvuruga nchi.
Masaju
amewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kutii mamlaka za dola
ikiwemo Jeshi la Polisi na mahakama iliyowapa mwongozo juu ya ombi la
kupinga zuio la jeshi la polisi na pia kufuata ushauri waliopewa na Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora juu ya kutokuwepo kwa udikteta
nchini.
Amesema
sababu kuu za kuzuia Oparesheni ni mbili ambazo ni hali ya usalama
kutokuwa shwari, pamoja na kutokuwepo kwa udikteta nchini.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )