Mfalme
wa muziki wa taarabu mzee Yusuph maarufu kama "mfalme wa taarabu"
amefunguka na kusema kuwa sasa ameamua kuachana na muziki huo na
kumrudia Mungu huku akiwataka watanzania pia kumrudia Mungu.
Akiongea jana baada ya kumaliza swala ya Ijumaa kweneye msikiti wa Ilala Bungoni (Masjdi Taqwa) Mzee
Yusuph alisema kwa taarifa za awali watanzania wanatakiwa kutambua kuwa
yeye ameachana na muziki na sasa amemrudia Mungu na kuwataka kuwa na
subira kwani atatafuta siku maalum yeye kutangaza suala hilo ambapo
atafunguka kwa kirefu zaidi kwanini ameamua kufanya maamuzi hayo.
"Ni
kweli nimeamua kuachana na muziki na sasa nimemrudia Mungu, nawaomba
watanzania wengine pia wamrudie Mungu, nitatafuta siku ambayo nitaongea
kwa kirefu zaidi juu ya suala hili, hivyo watanzania watambue tu
nimeachana na muziki sasa" alisema Mzee Yusuph.
Hii
ni mara ya pili kwa mzee Yusuph kutangaza kuacha muziki kwa mara ya
kwanza ilikuwa mwaka jana, alitangaza kuacha muziki na kuingia kwenye
siasa lakini hakuweza kufanya vizuri kwenye siasa na kurudi tena kwenye
muziki.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )